Jumuiya ya Watetezi wa Imani - Community of Faith Defenders
(CFDs) ni moja ya Idara ndani ya kanisa la Pentecostal Holiness Mission (PHM)
yenye malengo chanya kwa kanisa kama Idara zingine. Hii ni idara ambayo
inayohusisha vijana kuanzia umri wa miaka 15 hadi 50. Idara ya CFDs katika
utendaji wa kazi imegawanyika katika ngazi nne, kuanzia ngazi ya chini yaani kanisa
la mahali hadi ngazi ya juu ya kitaifa kama ifuatavyo:- CFDs katika kanisa la
mahali, Sehemu (Section), Jimbo na Taifa.
Idara ya CFDs kwa kipindi cha miaka kumi (10) kuanzia mwaka
2017 hadi 2027 imekuwa na malengo makuu kadha ya kimkakati. Katika utekelezaji
wake wa majukumu hayo ya kimkakati, CFDs unahusisha uongozi wa Taifa, Majimbo,
Sehemu, Makanisa ya mahali na wana CFDs wote kwa ujumula nchini. Ili
kulifanikisha zoezi zima hili tumesimamia kauli mbiu yetu inayosema “Mabadiliko
ya kiroho na kiuchumi katika PHM na CFDs inawezekana!! Wajibika!!” Lengo likiwa
ni kuwajibika ipasavyo kwa kila mwana Idara kupitia uongozi uliopo ili kuleta
maendeleo yenye tija ndani ya Idara. Hii ni kulingana na vipaumbele maalumu vya
utekelezaji vya kimkakati vilivyowekwa kwa miaka hiyo. Hali hii inalenga ukuaji
wa kanisa kiroho na kiuchumi kwa kutumia rasilimali zilizopo kwa ufanisi zaidi.
====================================================================
PENTECOSTAL HOLINESS MISSION
COMMUNITY OF FAITH DEFENDERS (CFDs)
(JUMUIYA YA WATETEZI WA IMANI)
HEADQUATERS
OFFICE CORNER
MOROGORO/MABIBO ROAD
P.O.BOX. 22503
DAR ES SALAAM
TANZANIA
TEL +255 222 401225
MOB: +255 765
413238
EMAIL phmcfdstaifa@yahoo.com or
phmacfdstaifa@gmail.com

No comments:
Post a Comment